SYRIA-USALAMA

Bashar al-Assad: Vita havijakoma nchini

Rais wa Syria Bashar al-Assad wakati wa mkutano na viongozi wa waliochaguliwa kutoka mikoa yote ya Syria, damascus, Jumapili hii, Februari 17, 2019.
Rais wa Syria Bashar al-Assad wakati wa mkutano na viongozi wa waliochaguliwa kutoka mikoa yote ya Syria, damascus, Jumapili hii, Februari 17, 2019. SANA/Handout via REUTERS

Rais wa Syria Bashar al-Assad ametangaza kwamba vita bado vinaendelea nchini mwake, huku akionya Wakurdi, bila hata hivyo kuwataja, kwamba majeshi ya Marekani ambao wanajiandaa kuondoka Syria, hayatawalindia usalama.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na viongozi wa waliochaguliwa kutoka mikoa yaote ya Syria, Bashar al-Assad amesema nchi yake inaendesha "aina nne za vita": kijeshi, kiuchumi, kimtandao na vita dhi ya rushwa.

Wakati huo huo Bashar al-Assad amewatahadharisha Wakurdi, bila hata hivyo kuwataja, kwamba wasitegemei tena msaada kutoka Marekani, huku akiwasihi kujishusha, na kujisalimisha kwani Marekani haitowalindia tena usalama wao.

Serikali ya Syria pekee ndio inaweza kuwaletea usalama na amani, amesema Bashar al-Assad.

Bw al Assad amemshutumu vikali rais wa Uturuki ambaye alimtaja kuwa ni mwanachama wa kundi la "Brotherhood". Recep Tayyip Erdogan ni "afisa tu mdogo wa Marekani na anaunga mkono Washington imuwezeshe kuingia kaskazini mwa Syria," amesema. Kiongozi wa Syria amekosoa mpango wa kuigawa nchi yakena mkoa wa Levant, akisema kuwa mpango huo sio mpya.

"Watumwa wa Uturuki"

Maneno haya yanakuja wakati Uturuki ilisema katika wiki za hivi karibuni nia yake ya kuanzisha eneo la usalama kwenye mpaka wa kilomita 30 katika eneo la Syria. "Kama hamko tayari kulinda nchi yenu, mtaendelea kuwa watumwa wa Uturuki," amesema al-Assad, akiwaambia wakazi wa kaskazini-mashariki mwa Syria, eneo linalodhibitiwa na Wanamgambo wa Kikurdi wanaosaidiwa na serikali ya Ankara.