ISRAELI-PALESTINA-USHIRIKIANO

Israeli yazuia msaada wa Dola Milioni 138 kwa Wapalestina

Chama cha PLO cha Abbaskimelaani "uamuzi mbaya" uliochukuliwa na serikali ya Israel.
Chama cha PLO cha Abbaskimelaani "uamuzi mbaya" uliochukuliwa na serikali ya Israel. REUTERS/Mohamad Torokman

Kwa mujibu wa serikali ya Benjamin Netanyahu, fedha hizi zinahusiana na posho iliyotolewa mnamo mwaka 2018 na Serikali ya Palestina kwa "magaidi wanaozuiliwa jela, kwa familia zao na kwa wafungwa wa zamani." Uamuzi ambao umepingwa vikali na viongozi wa Palestina.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili Israeli ilitangaza nia yake ya kuzuia dola Milioni 138 (sawa na Euro milioni 122) ambazo zingelipwa Wapalestina.

Kwa mujibu wa mamlaka ya Israel, fedha hizi zinalingana na posho ya iliyotolewa mnamo mwaka 2018 na Serikali ya Palestina kwa "magaidi wanaozuliwa jela, familia zao na wafungwa wa zamani."

Serikali ya Israeli inalipa mara kwa mara malipo ya VAT kwa Mamlaka ya Palestina na ushuru wa forodha inayotoza kwenye bidhaa zilizoagizwa na Wapalestina. Lakini mnamo mwezi Julai 2018, Bunge la Israel lilipitisha sheria inayozuia malipo ya kiasi hicho cha posho kilichotolewa na Serikali ya Palestina kwa wahusika wa mashambulizi dhidi ya Israel na familia zao.

"Huu ni uamuzi mbaya uliochukuliwa na serikali ya Israel" Saeb Erekat, namba 2 wa Palestina Liberation Organisation (PLO) ameiambia RFI, tunalaani vikali.