MAREKANI-SAUDIA-YEMEN-USALAMA-USHIRIKIANO

Muungano wa Kiarabu Yemen kupoteza uungwaji mkono kutoka Marekani

Uhusiano kati ya Marekani na Saudi Arabia uliingiliwa kasoro kufuatia kutowekwa kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, Oktoba 19, 2018!
Uhusiano kati ya Marekani na Saudi Arabia uliingiliwa kasoro kufuatia kutowekwa kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, Oktoba 19, 2018! REUTERS/Faisal Al Nasser

Bunge la Seneti la Marekani linatarajia kupiga kura Jumatao wiki hii kuhusu azimio linaloitaka Marekani kusitisha maramoja kuunga mkono muungano wa KIrabu unaoongozwa na Saudi Arabia katika mapigano dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Baraza la Wawakilishi linamtaka rais Donald Trump kuchukua msimamo mkali dhidi ya Suadi Arabia.

Azimio kama hilo liliwahi kupitishwa na Bunge la Seneti mwezi Desemba mwaka uliyopita lakini likazuiwa katika Baraza la Wawakilishi, ambapo wabunge kutoka chama cha Republican walikuwa wengi.

Bunge la Seneti lilionesha msimamo wake dhidi ya Donald Trump kwa kutambua pia kuwa Mwamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman alihusika katika mauaji ya mwandishi wa habari na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Kifalme nchini humo, Jamal Khashoggi.

Donald Trump alionya kwamba atatumia kura yake veto ikiwa azimio hilo litapitishwa.

Ili azimio hilo lianze kutumika, litatakiwa kupitishwa na taasisi zote mbili (bunge la Seneti na baraza la Wawakilishi), na kupata angalau theluthi mbili ya kura ili kuzuia kura ya veto ya rais Trump.

Maseneta wanatarajia kutuma ujumbe mzito kwa Saudi Arabia kwa kuhusika kwake katika mgogoro wa kibinadamu nchini Yemen na kwa mauaji ya Jamal Khashoggi.

Utawala wa Trump, pamoja na maseneta wengi kutoak chama cha Republican, wanaona kuwa azimio hilo halihitajiki, kwa sababu Marekani haishiriki katika vita nchini Yemen.

Hivi karibuni Donald Trump alisisitiza umuhimu wa uhusiano kati ya Marekani na Saudi Arabia, na jukumu la Saudi Arabia katika utulivu wa kanda ya mashariki ya Kati.