Pata taarifa kuu
SYRIA-OSDH-HAKI-USALAMA

OSDH: Zaidi ya watu 370,000 wameuawa tangu mwaka 2011 Syria

Mashambulizi ya majeshi ya muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani katika ngome ya mwisho ya IS ya Baghouz (Syria), Machi 11, 2019.
Mashambulizi ya majeshi ya muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani katika ngome ya mwisho ya IS ya Baghouz (Syria), Machi 11, 2019. © AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Zaidi ya watu 370,000 wameuawa tangu kuanza kwa vita nchini Syria ambavyo leo Ijumaa vinaingia mwaka wake wa tisa, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH).

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwao, raia wa kawaida 112,623, ikiwa ni pamoja na zaidi ya watoto 21,000 na wanawake 13,000, kwa mujibu wa shirika hilo.

Hali hiyo ilisababishwa na ukandamizaji wa kikatili uliofanywa na utawala kwa kuzima maandamano ya amani yanayounga mkono demokrasia.

Machafuko nchini Syria yalibadilika baada ya miaka kadhaa na kuwa kubwa ambavyo vimehusisha makundi ya waasi, makundi ya kijihadi na vikosi vya kigeni katika nchi hiyo ambayo imegawanyika.

Ripoti ya hivi karibuni mnamo mwezi Septemba iliyotolewa na OSDH iliripoti vifo vya watu zaidi ya 360,000.

Zaidi ya askari 125,000 wa jeshi la Syria na wanamgambo wanaounga mkono jeshi hilo wameuawa, kulingana na ripoti mpya ya OSDH. Aidha, wapiganaji 67,000 kutoka makundi mengine mbalimbali, ikiwa ni pamoja na waasi na wapiganaji wa Kikurdi, waliuawa, kwa mujibu wa OSDH.

Karibu wanajihadi 66,000, hasa kutoka kundi la Islamic State kundi (IS) na Hayat Tahrir al-Sham (HRT), tawi la zamani la Al Qaeda nchini Syria, pia waliuawa, chanzo hicho kimesema.

Mgogoro huo ulisababisha pia mamilioni ya raia wa Syria kuyahama makazi yao na kiukimbilia nchi za kigeni.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.