ISRAELI-PALESTINA-USALAMA

Watu sita wajeruhiwa baada ya roketi kurushwa Israeli

Roketi hiyo ilianguka mapema asubuhi juu ya nyumba huko Mishmeret, kaskazini mwa Tel Aviv.
Roketi hiyo ilianguka mapema asubuhi juu ya nyumba huko Mishmeret, kaskazini mwa Tel Aviv. REUTERS/Yair Sagi

Watu sita wamejeruhiwa baada ya roketi ya masafa marefu kurushwa katikati mwa Israeli. Roketi hiyo ilirushwa kutoka Ukanda wa Gaza, mamlaka nchini Israel imesema.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu anatazamiwa kufupisha ziara yake nchini Marekani ambayo alianza tangu siku ya Jumapili baada ya mazungumzo na Donald Trump.

"Kufuatia matukio ya usalama, nimeamua kufupisha ziara yangu nchini Marekani," Waziri Mkuu wa Israel amesema. Netanyahu, ambaye anatarajia kuwania muhula mwingine ifikapo Aprili 9, ameahidi kujibu kwa haraka mashambulizi hayo, ambayo ameyataja kama uhalifu usiokubalika.

Roketi hiyo ilianguka mapema asubuhi juu ya nyumba huko Mishmeret, kaskazini mwa Tel Aviv.

Tel Aviv na viunga vyake havijashuhudia mashamblizi ya roketi tangu Israeli ilipovamia eneo la Palestina mnamo mwaka 2014, eneo linalo dhibitiwa tangu mwaka 2007 na wapiganaji wa Kiislamu wa Hamas, ambapo mvutano bado unaendelea. Maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa Haki ya Wakimbizi wa mwaka 1948 kurudi nyumbani yatafanyika mwishoni mwa wiki hii.

Mtoto mchanga ni miongoni mwa watu sita waliojeruhiwa, wamesema maafisa wa idara ya hali ya dharura ya Magen David Adom. Picha zilizorushwa kwenye televisheni zinaonyesha jengo lililoharibiwa vibaya.

Machi 14, roketi mbili zilrushwa katika mji wa Tel Aviv, lakini hazikusababisha uharibifu wala hasara yoyote, kwa mujibu wa mamlaka ya Israel, ambayo ilishtumu kundi la Hamas.