ISRAELI-SIASA-NETANYAHU

Netanyahu aahidi kuongeza makaazi katika ukingo wa Magharibi

Waziri Mkuu wa Israel  Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Reuters

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema, ataendeleza makaazi ya walowezi katika eneo la ukingo wa Magharibi iwapo atachaguliwa tena kuongoza nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Ametoa ahadi hii kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika siku ya Jumanne wiki ijayo.

Maakazi hayo yapo kinyume na sheria za Kimataifa lakini Israel imekuwa ikipinga sheria hiyo.

Makaazi hayo yamesalia mojawapo ya mzozo kati ya Israel na Palestina, kutokana mzozo wa ardhi ambayo Palestina inasema Israel imechukua ardhi yake.

Netanyahu alikuwa Waziri Mkuu kwa muhula wa pili mwaka 2009, baada ya kuongoza awali akiongoza kati ya mwaka 1996 hadi 1999.

Mwaka 2015, alifanikiwa kushinda tena na kuunda serikali akishirikiana na washika wake wa karibu hasa wa vyama vinavyoegemea upande wa dini.