PALESTINA. GAZA-ISRAELI-USALAMA

Makundi yenye silaha ya Palestina yakubali kusitisha mapigano

Magari ya kijeshi ya israeli yakiwa yameegeshwa karibu na mpaka kati ya Israeli na Ukanda wa Gaza, Mei 6, 2019.
Magari ya kijeshi ya israeli yakiwa yameegeshwa karibu na mpaka kati ya Israeli na Ukanda wa Gaza, Mei 6, 2019. REUTERS/Ronen Zvulun

Makundi yenye silaha yamekubali kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza. Hatua hiyo ilifikiwa Jumapili usiku baada machafuko ya siku mbili, maafisa watatu kutoka Misri na Wapalestina wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kusitisha mapigano imeanza kutumika saa 4:30 asubuhi (saa saba na nusu usiku saa za kimataifa), afisa wa kundi la Hamas na mwingine kutoka kundi kundi la Islamic Jihad, ambaye hakutaja jina lake, wameliambia shirika la habari la AFP.

Afisa wa Misri pia amethibitisha taarifa hiyo, wakati msemaji wa jeshi la Israeli hakutaka kusema chochote.

Misri, kwa mara nyingine tena, ndio imesimamia usuluhishi.

Mapigano katika Ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya watu wengi na maelfu wengine kulazimika kuyatoroka makaazi yao.