SYRIA-USALAMA

Watu wengi wauawa katika mashambulizi ya jeshi Syria

Wapiganaji ishirini na sita wameuawa katika mapigano kati ya vikosi vya serikali vya Syria na wanamgambo wa kijihadi Jumatatu (Mei 6), Kaskazini Magharibi mwa Syria, ambako utawala na mshirika wake Urusi, wameongeza mashambulizi ya angani katika siku za hivi karibuni.

Watu wakitoroka makazi yao kufuatia mashambulizi ya anga na mapigano katika mikoa ya Hama na Idleb, Mei 1, 2019.
Watu wakitoroka makazi yao kufuatia mashambulizi ya anga na mapigano katika mikoa ya Hama na Idleb, Mei 1, 2019. Aaref WATAD / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Syria limesonga mbele kaskazini magharibi mwa mkoa wa Hama baada ya mapigano makali na kundi la Hayaat Tahrir al-Sham, tawi la zamani la kundi la Al-Qaida nchini Syria, na mshiriki wake, Chama cha Kiislamu cha Turkistan.

Chama hiki kinaundwa na wapiganaji wa Uygur kutoka China na watu kutoka Jamhuri za zamani za Soviet ya Asia ya Kati.

Majeshi ya Serikali yameweza kuchukua udhibiti wa kijiji ch kimkakati cha Tall Osman, ambacho ni jirani na eneo kubwa linalodhibitiwa na wanamgambo wa kijihadi baada ya kushambuliwa kwa makombora na vita vya chini kwa chini.

Hii ni mara ya kwanza jeshi la Syriakusonga mbele tangu kutekelezwa kwa mkataba wa kusitisha mapigano katika mkoa huo Septemba mwaka jana kwa msaada wa Urusi na Uturuki. Lakini katika siku za hivi karibuni, ndege za jeshi la Urusi zimeongeza mashambulizi dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na wanamgambo wa kijihadi.

Hivi karibuni ndege zimeharibu mali nyingi, ikiwa ni pamoja na hospitali na majengo mengine ya serikali, na kusababisha maelfu ya raia kutoroka makazi yao.