AFGHANISTANI-TALIBAN-USALAMA

Makao makuu ya shirika la kihisani yashambuliwa Kabul

Watu wenye silaha wameshambulia makao makuu ya shirika la kihisani la Counterpart International jijini Kabul, nchini Afghanistan leo Jumatano, mamlaka nchini Afghanistan imesema.

Watu 24 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.
Watu 24 wamejeruhiwa katika shambulio hilo. REUTERS/Mohammad Ismail
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi ambalo, limedaiwa kutekelezwa na kundi la Taliban, limesababisha takriban ishirini kujeruhiwa.

Washambuliaji wamelipua bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari ndogo kabla ya kuvamia jengo la shirika la Counterpaart International katika eneo la Shahr Naw.

Vikosi maalum, vikishirikiana na washauri wa kigeni wametumwa katika eneo la shambulio ili kuwaondoa washambuliaji katika jengo hilo. Eneo lote limezingirwa na milipuko pamoja na milio ya risasi vimesikika,

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Nasrat Rahimi amesema wafanyakazi 80 wa shirika la Counterpart International waliondolewa na kuweka eneo salama.

Operesheni ya kuondoa wafanyakazi kwenye jengo ambalo ni makao makuu ya shirika la Counterpart International inaendelea kwa umakini wa hali ya juu, " amesema Nasrat Rahimi.

Watu tisa miongoni mwa majeruhi wamepelekwa hospitali, Wizara ya Afya imebaini, Hata hivyo chanzo cha hospitali kimsem awatu kumi na tano wamejeruhiwa.

Zabihullah Mujahid, msemaji wa kundi la Taliban, amekiri kuwa shambulio limeendeshwa na Taliban, akishtumu shirika hilo kushirikiana na serikali ya Kabul ili kuendeleza sera mbaya dhidi ya Uislam.

Counterpart International, shirika ambalo limeanzishwa nchini Marekani, liko nchini Afghanistan tangu 2005.