PAKISTAN-MAUAJI-USALAMA

Watu wengi waangamia katika mlipuko karibu na Lahore

Maofisa wa polisi katika eneo la mlipuko karibu na msikiti wa Sufi, Mei 8, 2019 Lahore, Pakistan.
Maofisa wa polisi katika eneo la mlipuko karibu na msikiti wa Sufi, Mei 8, 2019 Lahore, Pakistan. © AFP

Mlipuko uliolenga vikosi vya polisi karibu na msikiti wa Sufi katika jiji la kaskazini-mashariki mwa Pakistan la Lahore, umeua watu zaidi ya kumi na wengine 24 kujeruhiwa, vyanzo vya polisi vimesema.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa polisi wa Lahore amesema mlipuko ulitokea karibu na eneo la Data Darbar, mojawapo ya maeneo muhimu katika Asia ya Kusini.

"lilikuwa ni shambulio dhidi ya polisi ambalo limeua watu wengi na maafisa kadhaa wa polisi na raia wamejeruhiwa," amesema Syed Mubashir Hussain.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Pakistan, watu 10 ndio wameuawa katika shambulio hilo.

Shughuli ya uokoaji inaendelea na watu 15 wamepelekwa hospitali, amesema msemaji wa idara ya huduma za dharura katika mji wa Lahore.

Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo baya kuwahi kutokea tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan nchini Pakistan.