SYRIA-USALAMA

Wanajihadi na waasi wafanya mashambulizi makubwa katika Mkoa wa Latakia

Ndege za kivita za KUrusi zikipaa juu ya jiji la Latakia, ngome kuu ya ukoo wa Assad. (picha ya kumbukumbu)
Ndege za kivita za KUrusi zikipaa juu ya jiji la Latakia, ngome kuu ya ukoo wa Assad. (picha ya kumbukumbu) REUTERS/Omar Sanadiki

Kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, wanajihadi na waasi wamezindua mashambulizi makubwa katika milima ya mkoa wa pwani wa Latakia.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano yalishuhudiwa kwa siku nzima ya Jumanne Julai 9 na gharimu maisha ya watu 35 katika pande zote mbili, kulingana na shirika la Haki za Binadamu nchini Syriala OSDH.

Tangu kuanza kwa mashambulizi yake dhidi ya maeneo ambayo bado halijadhibiti, kaskazini magharibi mwa Syria, Aprili 30, jeshi la Syria lilijaribu bila mafanikio kuwatimua wanajihadi na waasi wanaoungwa mkono na Uturuki kwenye ngome yao. katika Mkoa wa wenye milima wa Latakia.

Pamoja na matumizi yenye uwezo wa nguvu na majeshi mengi yaliyotumwa, jeshi la serikali, linaloungwa mkono na ndege za kivita za Urusi, limeshindwa kusonga mbele hadi Jabal Turkman.

Mlima wa Jabal Turkman ni mwiba kwa jeshi la Syria kuweza kudhibiti au kupenya kuingia katika mkoa wa Latakia.