AFGHANISTANI-TALIBAN-USALAMA

Ishirini na nane waangamia katika mlipuko wa basi Afghanistani

Vikosi vya Afghanistan vikitoa ulinzi mkali katika eneo la shambulio.
Vikosi vya Afghanistan vikitoa ulinzi mkali katika eneo la shambulio. REUTERS/Mohammad Ismail

Watu zaidi ya 28, "hasa wanawake na watoto," wameuawa mapema Jumatano hii asubuhi magharibi mwa Afghanistan wakati basi lao lilikanyaga bomu la ardhini lililotegwa kando ya barabara "na wapiganaji wa Taliban", mamlaka imesema.

Matangazo ya kibiashara

"Mapema asubuhi basi lililokuwa likisafiri kati ya Kandahar na Herat limekanyaga bomu lililotegwa na wapiganaji wa Taliban kando na barabara. Kwa sasa watu wasiopungua 28 ndio wamepoteza maisha na 10 wamejeruhiwa," amesema msemaji wa polisi katika mkoa wa Farah, magharibi mwa nchi, Muhibullah Muhib.

Kwa mujibu wa Bw Muhib, vikosi vya usalama ndio vimekuwa vimelengwa na bomu hilo.

Ofisi ya gavana wa Farahimeithibitisha idadi hiyo ya watu waliouawa, lakini imeonya kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka.

Mpaka sasa kundi la Taliban halijazungumza chochote kuhusiana na tukio hilo baya.

Vifo hivi vinatokea siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kuchapisha ripoti ambayo inelezea masikitiko yake kuwa raia wanaendelea kuuawa na kujeruhiwa kwa idadi kubwa "isiyokubalika" licha ya mazungumzo yanayolenga kumaliza miongo kadhaa ya vita.

Licha ya kupungua kwa asilimia 27 kwa idadi ya watu waliouawa katika kipindi cha kwanza chamwaka 2019 ikilinganishwa na miezi sita ya kwanza ya mwaka 2018, raia 1,366 waliuawa na 2,446 walijeruhiwa, Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (Manua) imebaini katika ripoti yake ya nusu ya mwaka.

Theluthi moja ya waathiriwa hao ni watoto (vifo 327 na 880 waliojeruhiwa).

Manua imeripoti kwamba raia zaidi waliuawa na vikosi vya serikali kuliko makundi yawaasi (vifo 717 dhidi ya 531), kwa kiasi kikubwa kutokana na mashambulizi ya anga ya jeshi la Afghanistan na Marekani.