AFGHANISTANI-TALIBAN-SIASA-USALAMA

Taliban yatishia kuvuruga uchaguzi wa urais

Vikosi vya usalama vya Afghanistan vikipiga kambi karibu na eneo la shambulizi dhidi ya makao makuu ya shirika la kihisani Kutoka Marekani, Kabul Jumatano, Mei 8, 2019.
Vikosi vya usalama vya Afghanistan vikipiga kambi karibu na eneo la shambulizi dhidi ya makao makuu ya shirika la kihisani Kutoka Marekani, Kabul Jumatano, Mei 8, 2019. REUTERS/Mohammad Ismail

Kundi la Taliban limetoa witoa kwa wananchi wa Afghanistan kususia shughuli za serikali na kutishia kuvuruga uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo pia limewataka wananchi wa Afghanistan kuepuka mikusanyiko "ambayo inaweze kulengwa.

"Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa Taliban, Zabiullah Mujahid, kundi hilo "limeomba" wapiganaji wao kupinga "mchakato huo wa uchaguzi kwa namna wanavyoweza".

"Ili kuzuia wananchi wetu wasipate hasara, Mungu atuepushe, wanapaswa kuepuka mikusanyiko ambayo inaweza kulengwa kwa wakati wowote," Taliban imetishia.

Tangazo hilo linakuja wakati Marekani na wawakilishi wa Taliban wanaendelea na kikao cha nane cha mazungumzo katika mji wa Doha. Mjumbe wa Marekani Zalmay Khalilzad amekaribisha Jumatatu jioni "hatua ambayo mazungumzo kati ya pande hizo mbil yamefikia".

Mazungumzo ya amani kati ya Taliban na Marekani, Doha, Qatar, Februari 26, 2019.
Mazungumzo ya amani kati ya Taliban na Marekani, Doha, Qatar, Februari 26, 2019. Qatari Foreign Ministry/Handout via REUTERS

Katika mahojiano na shirika la Habari la AFP, msemaji wa kisiasa wa Taliban Suhail Shaheen, pia alisema Jumanne kwamba wamefikia "hatua kubwa" katika mazungumzo yao.

Tunajadili hoja za mwisho na mkataba wa amani utafikiwa. Tutaamua tarehe ya kutangazwa kwa mkataba huo," amesema. Kampeni ya uchaguzi wa urais ilifunguliwa rasmi Julai 28 nchini Afghanistan.