AFGHANISTANI-USALAMA

Afghanistan: Mlipuko wasababisha hasara kubwa Kabul

Maafisa wa polisi wa Afghanistan wakipiga kambi karibu na eneo la mlipuko Kabul Agosti 7, 2019.
Maafisa wa polisi wa Afghanistan wakipiga kambi karibu na eneo la mlipuko Kabul Agosti 7, 2019. REUTERS/Omar Sobhani

Karibu watu 80 wamejeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotegwa katika gari leo Jumatano asubuhi, shambulio ambalo lilmetokea magharibi mwa mji mkuu wa Afghanistani, Kabul, maafisa na mashahidi wamesema.

Matangazo ya kibiashara

"Nimesikia mlipuko mkubwa na madirisha yote ya duka langu yameharibika," Ahmad Saleh, mfanyabiasaha, ameliambia shirika la Habari la AFP.

"Bado ninachanganyikiwa na sijui kilichotokea, lakini vio vya madirisha ya maduka kadhaa, ambayo baadhi yanapatikana kilomita moja kutoka eneo la mlipuko, vimevunjika," ameongeza.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Nasrat Rahimi, "gari iliyojaa mabomu ililipuka mbele ya lango la kituo cha polisi magharibi mwa Kabul saa 9:00 asubuhi (sawa na saa 12 asubuhi saa za Afrika ya Kati)", bila kutoa maelezo zaidi.

Kulingana na video inayoonekana kwenye mitandao ya kijamii na kwa mujibu wa mashahidi, milio ya risasi imesikika baada ya mlipuko huo.

Karibu watu 34 wamepelekwa katika hospitali za mji huo, msemaji wa Wizara ya Afya Wahidullah Mayar almesema.

Vurugu hizo ziliongezeka ka kiasi kikubwa mwezi Julai, mwezi ambapo watu wengi waliuawa tangu Mei 2017, ambapo watu zaidi ya 1,500 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.