SAUDIA-HIJA-UISLAMU

Ibada kubwa ya Hija yaanza Makka katika hali ya mvutano Ghuba

Mahujaji kwenye Msikiti Mkubwa wa Makka, Agosti 7, 2019.
Mahujaji kwenye Msikiti Mkubwa wa Makka, Agosti 7, 2019. REUTERS/Waleed Ali

Hija, ibada ya kila mwaka kwa Waislamu kutimiza nguzo ya tano ya Uislamu, inaanza Ijumaa hii, Agosti 9, nchini Saudi Arabia. Ni moja ya mkusanyiko mkubwa wa kidini ulimwenguni: Waislamu zaidi ya milioni 2 wanatarajiwa kushiriki ibada hiyo, katika hali ya mvutano mkubwa katika eneo la Ghuba.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi dhidi ya meli za mafuta katika eneo la Ghuba, huku Saudi Arabia ikishutumu hasimu wake mkubwa Iran kuhusika na uhasama huo, wakati serikali ya Tehran ikikanusha; Tehran pia inanyoonshewa kidole na Marekani...

Mvutano umeongezeka katika Ghuba ya Uajemi ...Lakini mvutano huo katika Ghuba haukuzuia raia 88,550 wa Iran kwenda Makka, kushiriki ibada ya hija. Raia wa Irani ni miongoni mwa Waislamu wanaoshiriki ibada ya Hija kwa idadi kubwa, baada ya Indonesia, Pakistanis na India.

Kila Mwislamu ana jukumu la kufanya Hija mara moja katika maisha yake, ikiwa ana uwezo. Makka ni mji mtakatifu ambapo, kulingana na kitabu kitakatifu cha Qoran, ulizaliwa Uislamu na mtume Muhammad. Kila mwaka, waumini na kwenda kufanya mfululizo wa ibada maalum kwa siku 5.