LEBANON-ISRAELI-USALAMA

Lebanon: Hezbollah wadai kuangusha ndege isoyo na rubani ya Israeli

Hassan Nasrallah, kiongozi wa kundi la Hezbollah, Lebanon, Desemba 7, 2017.
Hassan Nasrallah, kiongozi wa kundi la Hezbollah, Lebanon, Desemba 7, 2017. Handout / AL-MANAR TV / AFP

Kundi la Hezbollah limetangaza leo Jumatatu kwamba limeangusha "ndege isiyo na rubani ya Israeli" wakati imekua ikijaribu kuvuka mpaka wa Lebanon, wiki moja baada ya mzozo mdogo kati ya kundi hili la Kiahia na serikali ya Kiyahudi.

Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji wa Hezbollah "walikabiliana na silaha zinazohitajika, ndege isiyo na rubani ya Israeli wakati imekuwa ikijaribu kuvuka mpaka kati ya Palestina na Lebanon kuelekea mji wa Ramieh" kusini mwa Lebanon, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwakundi la Hezbolaah. "ndege isiyo na rubani ilidondoshwa nje ya eneo hilo na iko mikononi mwa Hezbollah," kulingana na taaifa hiyo.

Lakini Israeli haijasem chochote kuhusiana na madai haya ya Hezbollah.

Hivi karibuni kuliibuka mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hezbollah.

Shambulio la Israel dhidi ya kituo cha Hezbollah cha Dahiya huko Beirut - lilichangia makabiliano haya ya mpakani. Hili lilitazamwa na wachambuzi wa jeshi kama "ukiukaji wa sheria za mchezo".

Hili lilikuwa shambulio la kwanza la Israeli katika mji mkuu wa Lebanon tangu kuzuka vita baina ya Israel na Hezbollah mnamo 2006. Makabiliano ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili kwa kawaida huwa ni nadra.

Wachambuzi wanasema kinachoendelea hapa ni vita ambavyo havijatangazwa sio tu baina ya Israel na Hezbollah, lakini pia baina ya Israel na mfadhili wa Hezbollah, Iran.

Hezbollah, tafisri yake ni "chama cha Allah" ni chama cha siasa kinachofuata nadharia za Kishia chenye makao yake nchini Lebanon. Kiliibuka baada ya Israel kuivamia Lebanon mwaka 1982, na kinafungamana na Iran.

Hezbollah imeshutumiwa kwa kufanya mashambulizi na njama dhidi ya maeneo ya Israel. Linachukuliwa kuwa kundi la kigaidi na mataifa ya Magharibi, Israeli, mataifa ya Kiarabu ya kanda ya Ghuba na Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu (Arab League).

Hata hivyo kundi hilo limetoa mchango mkubwa katika siasa za Lebanon tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990na limeshiriki katika uchaguzi wa kitaifa.