MAREKANI-AFGHANISTANI-TALIBAN-USALAMA

Donald Trump avunja mazungumzo na Taliban

Donald Trump ametangaza kwamba mazungumzo na Taliban "yavumenjika moja kwa moja"
Donald Trump ametangaza kwamba mazungumzo na Taliban "yavumenjika moja kwa moja" REUTERS/Joshua Roberts

Rais wa Marekani, Donald Trump amethibitisha kwamba mazungumzo na Taliban "yamevunjika" baada ya kufutwa kwa mkutano wa siri uliopangwa kufanyika katika eneo la Camp David, ambapo wengi walifikiri kwamba hali hiyo itasababisha mvutano upande wa Washington.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Rais Donald Trump inaendana na ile ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, ambayo yalionyesha siku ya Jumapili uwezekano wa kuanza tena kwa mazungumzo na waasi wa Afghanistan. "Yamemalizika. Kwa kadiri ninavyofikiria, mazungumzo yamemalizika moja kwa moja, "Donald Trump amesema akiwa kwenye bustani ya White House, akizungumza kwa sauti ya kali.

Baada ya kuvunja mazungumzo haya, ambayo yalionekana kuwa kwenye hatua ya kufikia mkataba wa kihistoria baada ya miaka 18 ya vita, Donald Trump amehakikisha kwamba jeshi la Marekani limepunguza mashambulizi dhidi ya waasi wa Taliban, tangu kutokea kwa shambulizi baya Alhamisi wiki iliyopita katika mji wa Kabul, shambulizi ambalo liligharimu maisha ya askari mmoja wa Marekani.

"Katika siku nne zilizopita, tumewapiga vibaya adui zetu kuliko wakati wowote katika miaka kumi iliyopita," Donaled Trump amesema. "Kulikuwa na mkutano uliopangwa, ilikuwa wazo langu, na pia ilikuwa wazo langu kufuta. Sikujadili haya na mtu yeyote. Wakati niliposikia kwamba wamemuua mmoja wa askari zetu na watu kumi na wawili wasio na hatia, nilisema kwamba sintokubali kukutana nao kwa mazungumzo yoyote. Wmefanya makosa. "

Donald Trumpa aliulizwa kuhusu kuvunjika kwa mazungumzo hayo iwapo kunamaanisha kuondokana na mpango wa kuondoa polepole askari 13,000 hadi 14,000 wa Marekani nchini Afghanistan, kama ilivyokusudiwa katika makubaliano ambayo yalikuwa yakijadiliwa. Alijibu akianza kusema: "Tuna polisi nchini Afghanistan kwa muda mrefu, na serikali italazimika kuchukua majukumu. Tangu kampeni yangu nilisema tutaondoka nchini Afghanistani haraka iwezekanavyo. Nilipenda tuondoke nchini humo, lakini tutatekeleza mpango huo kwa wakati muafaka."