ISRAELI-UCHAGUZI-SIASA

Netanyahu atoa wito kwa Gantz kuunda serikali ya umoja

Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu (kushoto) akipeana mikono na mpinzani wake mkuu, Jenrali mstaafu Benny Gantz, Septemba 19, 2019, Jerusalem.
Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu (kushoto) akipeana mikono na mpinzani wake mkuu, Jenrali mstaafu Benny Gantz, Septemba 19, 2019, Jerusalem. © AFP

Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, ambaye anaendelea kubanwa kisiasa, amewashangaza wengi nchini Israeli, akitoa wito kwa Benny Gantz kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, siku mbili baada ya uchaguzi wa wabunge ambao vyama viwili vikuu vimeendelea kukabana koo.

Matangazo ya kibiashara

Jumatano usiku wiki hii, Netanyahu alisema kwamba Israeli ina hiari ya kuchagua mambo mawili: ama serikali ya mrengo wa kulia itayoongozwa na yeye au "serikali hatari itakayo kuwa chini ya vyama vyenye wafuasi wengi wa Kiarabu", kauli aliyotumia kwa kumshambulia moja kwa moja mpinzani wake Benny Gantz ambaye aliahidi kuanza mazungumzo ya wazi na vyama vyenye wafuasi wengi wa Kiarabu kwa matumaini ya kufikia muungano.

Kauli iliyowashangaza wengi: Waziri Mkuu, kwa aliendelea kukaa madarakani mfululizo kwa muongo mmoja, amebadilisha kauli yake na kupendekeza mazungumzo ya moja kwa moja na mpinzani wake mkuu, Jenerali mstaafu Benny Gantz.

"Wakati wa uchaguzi, nilitoa wito wa kuundwa kwa serikali ya mrengo wa kulia, lakini kwa bahati mbaya matokeo ya uchaguzi yanaonyesha kuwa hii haiwezekani. Watu hawakuamua vilivyo kati ya kambi hizo mbili. Kwa hiyo, hakuna budi ila kuunda serikali ya umoja, "Netanyahu amesema kwenye ujumbe wa video.

Benjamin Netanyahu na Benny Gantz wamesaliamiana na kupeana mikono katika hafla ya kumbukumbu ya miaka mitatu ya kifo cha Waziri Mkuu wa zamani na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Shimon Peres, iliyofanyika mjini Jerusalem leo Alhamisi, kwa mujibu wa mpiga picha wa shirika la Habari la AFP.

Siku mbili baada ya uchaguzi wa wabunge, matokeo ya muda yanaonyesha kwamba chama cha Benjamin Netanyahu, Likud kimepata viti 31 kati ya 120 vinavyohitajika katika Bunge la Israeli (Knesset), dhidi ya viti 33 kilivyopata chama cha Kahol Lavan ("Bluu na Nyeup") cha Benny Gantz.