Pata taarifa kuu
UTURUKI-SYRIA-MAREKANI-USALAMA

Uturuki yaanza operesheni ya kijeshi dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi Syria

Msafara wa magari ya jeshi la Uturuki, Akcakale, Oktoba 9, 2019.
Msafara wa magari ya jeshi la Uturuki, Akcakale, Oktoba 9, 2019. REUTERS TV via REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Uturuki imeanza kutekeleza ahadi yake licha ya nchi nyingi kupinga hatua hiyo katika siku mbili zilizopita. Jeshi la Uturuki lilizindua oparesheni yake ya kijeshi kaskazini mashariki mwa Syria Jumatano hii Oktoba 9. Rais Erdogan mwenyewe alitangaza kuanza kwa operesheni hiyo.

Matangazo ya kibiashara

"Vikosi vya Jeshi la Uturuki na wapiganaji kutoka Syria [wanaoungwa mkono na Ankara] wameanza operesheni inayoitwa" Chanzo cha Amani "kaskazini mwa Syria, Recep Tayyip Erdogan ametangaza katika ujumbe wa Twitter ulioandikwa kwa Kituruki, Kiingereza na Kiarabu.

Recep Tayyip Erdogan amesema, operesheni hii inalenga "magaidi wa YPG na IS" na inakusudia kuweka "eneo la usalama" kaskazini mashariki mwa Syria.

"Eneo la usalama ambalo tutaweka litawezesha wakimbizi wa Syria kurudi katika nchi yao," Bw Erdogan ameongeza. Wako zaidi ya milioni tatu na nusu nchini Uturuki. Mbali na kundi la wapiganaji wa Kikurdi, rais wa Uturuki ametaja kati ya malengo ya operesheni hiyo kulenga kundi la Islamic State - ujumbe ambao uliotumwa kwa Donald Trump.

Mwishowe, katika ujumbe wake, rais wa Uturuki pia amehakikisha kuwa operesheni hiyo "itaheshimu mipaka ya Syria", ujumbe ambao umetumwa kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin, mshirika mkubwa wa serikali ya Syria.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.