SYRIA-MAREKANI-UTURUKI-USALAMA

Mashambulizi ya Uturuki Syria: Marekani yawekea vikwazo wizara mbili za Uturuki

Donald Trump amemuomba Rais wa Uturuki aondoe vikosi vyake nchini Syria na atangaze kusitisha mapigano mara moja.
Donald Trump amemuomba Rais wa Uturuki aondoe vikosi vyake nchini Syria na atangaze kusitisha mapigano mara moja. REUTERS/Leah Millis

Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya Wizara mbili nchini Uturuki na maafisa watatu wa serikali, kutokana na operesheni ya kijeshi inayoendelea Kaskazini mwa Syria dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi.

Matangazo ya kibiashara

Makamu wa rais Mike Pence amesema, Rais Donald Trump amempigia simu mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na kumtaka asitishe operesheni hiyo.

Wakati huo huo, ripoti zinasema kuwa jeshi la Syria limeingua Kaskazini Mashariki mwa nchi hyo, hali ambayo inahofiwa kuwa huenda makabiliano yakashuhudiwa kati ya wanajeshi wa nchi hizo mbili.

Jeshi la Uturuki wiki iliyopita, lilianza operesheni ya kuwashambulia wapiganaji wa Kikurdi wanaosema ni maadui wake,wapiganaji ambao walishirikiana na wanajeshi wa Marekani dhidi ya kundi la Islamic State nchini Syria.