UFARANSA-IRAQ-USALAMA

Paris yafanya mazungumzo na Baghdad kuhusu kuhamishwa kwa wanajihadi

Wazir wa Mambo ya Nje wa Ufaransa,  Jean-Yves Le Drian.
Wazir wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian. REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian anajadili na viongozi wa Iraq kuhusu uwezekano wa kuwasafirisha wanajihadi wa kigeni na kuwahukumu nchini Iraq.

Matangazo ya kibiashara

Raia 60 Ufaransa, ni miongoni mwa wanajihadi wanaoshikiliwa na wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria, ambao wanalengwa na mashambulizi ya Uturuki, na hivyo kuongeza "hatari ya kutawanyika" kwa wapiganaji hao.

Tangu Ankara ilipozindua mashambulizi yake dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi nchini Syria Oktoba 9, nchi kadhaa za Ulaya ambazo zilikumbwa na mashambulizi mabaya, hususan Ufaransa, Ubelgiji na Ujerumani wana wasiwasi kwamba wanajihadi 12,000 wanaozuiliwa na wapiganaji wa Kikurdi ikiwa ni pamoja na wanajihadi 2,500 hadi 3,000 kutoka nchi za kigeni, wanawea kutoroka na kwenda kusaidia kundi la Islamic State, ambalo lilipoteza makao yake makuu mwezi Machi mwaka huu.

Leo Alhamisi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean Yves Le Drian atakutana na mwenzake wa Iraq Mohammed Ali al-Hakim, Rais Barham Saleh na Waziri Mkuu Adel Abdel Mahdi kwa lengo la kutafuta utaratibu wa kuweka mahakama itakayohukumu jumla ya wanajihadi wanaoshikiliwa, ikiwa ni pamoja wanajihadi kutoka Ufaransa", amesema waziri huyo wa Ufaransa .

Kufikia sasa, raia 14 wa Ufaransa wamehukumiwa na mahakam za Iraqi kwa kujiunga na kundi la ISlamic State. Kati ya hawa, 12 walihamishwa kutoka magereza ya wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria kwenda Baghdad. Kumi na moja walihukumiwa kifo na wengine watatu - ikiwa ni pamoja na wanawake wawili - walihukumiwa kufungo cha maisha.