SYRIA-UTURUKI-MAREKANI-USHIRIKIANO-USALAMA

Uturuki yakubali kusitisha mashambulizi Syria kuruhusu Wakurdi kuondoka

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence Oktoba 17, 2019, Ankara.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence Oktoba 17, 2019, Ankara. AFP/Shaun TANDON

Uturuki imekubali kusitisha operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi Kaskazini mwa nchi ya Syria. Wakati huo huo vyombo vya habari nchini Uturuki vimeendelea kuzungumzia kuhusu kitendo cha Rais Erdogan 'kuitupa pipani barua ya Trump kuhusu Syria '.

Matangazo ya kibiashara

Hii imekuja, baada ya ziara ya Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence jijini Ankara na kufanya mazungumzo na rais Recep Tayyip Erdogan.

Mapigano hayo yamesitishwa kwa muda wa siku tano, na Marekani itawasaidia wapiganaji wa Kikurdi kuondoka na kwenda katika sehemu salama.

Awali Urusi iliiahidi Uturuki kuwa, vikosi vya wanamgambo wa Kikurdi nchini Syria wa kundi la YPG havitakuwa kwenye maeneo ya mpaka ya Syria. Hayo ni kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya kigeni wa Uturuki Mevlut Cavusoglu.

Bw Cavusoglu amesema iwapo Urusi pamoja na jeshi la Syria watawaondoa wapiganaji wa YPG katika eneo hilo nchi yake haitopinga suala hilo.

Alhamisi wiki hii msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni wa Urusi alisema Syria inapaswa kudhibiti mpaka wake na Uturuki.