Pata taarifa kuu
UTURUKI-URUSI-SYRIA-USALAMA

Uturuki na Urusi kuanza doria ya pamoja Ijumaa Novemba 1

Rais wa Urusi Vladimir Putin (kulia) na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika mkutano na waandishi wa habari Sochi baada ya mazungumzo kuhusu Syria Oktoba 22, 2019.
Rais wa Urusi Vladimir Putin (kulia) na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika mkutano na waandishi wa habari Sochi baada ya mazungumzo kuhusu Syria Oktoba 22, 2019. Sergei CHIRIKOV / POOL / AFP

Majeshi ya Uturuki na Urusi yanatarajia kushiriki doria ya pamoja kuanzia Ijuma wiki wiki hii Kaskazini Mashariki mwa Syria ili kuruhusu wanamgambo wa Kikurdi kuondoka kwenye eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Doria hiyo ya pamoja inakuja kufuatia makubaliano ya kusimamisha mapigano yaliosimamiwa na Urusi yaliotaka wapiganaji wa Kikurdi kuondoka na kuelekea upande wa kusini ili kulifanya eneo la kaskazini kuwa eneo salama. 

Wakati huo huo Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameonya kuwa majeshi yake yako tayari kujibu mashambulizi yoyote dhidi ya Uturuki na ikiwa mapigano yataendelea, na kama wanamgambo hao watakuwa bado hawajaondoka wote kulingana na makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni.

“Uturuki pamoja na Urusi siku ya Ijumaa zitaanzisha doria ya pamoja Kaskazini Mashariki mwa Syria. Lakini Uturuki haitosita kuanzisha operesheni zake iwapo wapiganaji wa Kikurdi hawatokuwa wameondoka kilomita 30 kutoka eneo la kaskazini au iwapo kundi hilo litaanzisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya Uturuki“ Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema.

Hilo linatokea wakati kukiarifiwa mapigano makali kati ya vikosi vya Syria na Uturuki katika mji wa mpakani wa Ras al Ain ambako Uturuki inalenga kulifanya eneo lake salama. Uturuki ilianzisha operesheni za kijeshi kaskazini mashariki mwa Syria mapema mwezi huu kwa nia ya kuwaondoa wapiganaji wa Kikurdi wa Syria kutoka eneo hilo. Uturuki inaliona kundi hilo kama kundi la kigaidi linalofungamana na waasi waliopo nchini mwake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.