UTURUKI-URUSI

Uturuki na Urusi waanza doria ya pamoja nchini Syria

Wanajeshi wa Uturuki na Urusi wameanza kufanya doria ya pamoja kukagua ikiwa wapiganaji wa Kikurdi wameondoka kwenye maeneo muhimu ya mpakani hatua ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya nchi hizo mbili.

Magari ya jeshi la Marekani karibu na mji wa wakurdi wa Bardarash baada ya kujiondoa kutoka kaskazini mwa Syria mnamo Oct. 21
Magari ya jeshi la Marekani karibu na mji wa wakurdi wa Bardarash baada ya kujiondoa kutoka kaskazini mwa Syria mnamo Oct. 21 Safin Hamed/AFP/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Doria hiyo ambayo ilianza jana asubuhi, imekuja baada ya makubaliano ya juma lililopita kwenye mji wa Sochi, ambapo nchi hizo mbili zilikubaliana kuwa wapiganaji wa Kikurdi waondoke kwenye maeneo ya mpaka na Uturuki, ambapo Urusi imethibitisha kuondoka kwao.

Vikosi hivi vinaungana na wanajeshi wengine wa Marekani ambao juma lililopita rais wa Marekani Donald Trump aliagiza wanajeshi wake kusalia kulinda miundombinu ya mafuta.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya Ankara, imethibitisha kuondoka kwa wapiganaji hao na kuongeza kuwa doria hiyo itaendelea kwa majuma kadhaa ili kuhakikisha makubaliano yaliyofikiwa hayakiukwi.