MAREKANI-AFGHANISTANI-TALIBAN-USALAMA

Trump atangaza kuanza tena kwa mazungumzo na Taliban

Akizuru kambi ya kikosi cha jeshi la wanaanga la Marekani huko Bagram, Rais wa Marekani Donald Trump amekutana naRais wa Afghanistan Ashraf Ghani na kula chakula cha jioni na askari wa Marekani.
Akizuru kambi ya kikosi cha jeshi la wanaanga la Marekani huko Bagram, Rais wa Marekani Donald Trump amekutana naRais wa Afghanistan Ashraf Ghani na kula chakula cha jioni na askari wa Marekani. REUTERS/Tom Brenner

Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza wakati wa ziara yake ya kushtukiza usiku katika kambi ya kikosi cha jeshi la Marekani nchini Afghanistan kwamba mazungumzo na Taliban, yaliyositishwa mwezi Septemba, yameanza tena.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya Bw Trump, ambayo ni ya kwanza nchini humo, ilikuwa ya kushtukiza kwa sababu za usalama.

"Wataliban wanataka mkataba, na tunakutana nao, tumewaambia kuwa tunataka kusitishwa kwa mapigano, awali hawakutaka kusitisha mapigano, na sasa wanataka kusitisha mapigano," amesema Donald Trump baada ya kukutana na mwenzake wa Afghanistan Ashraf Ghani, katika kambi ya kikosi cha jeshi la wanaanga la Marekani ya Bagram, kilomita 80 kaskazini mwa Kabul.

"Nadhani kwa uhakika hii ni njia nzuri," amebaini rais wa Marekani.

"Tutasalia hivi mpaka mpale tutakuwa na mkataba au mpaka pale tutapata ushindi kamili, na wanataka kweli kufikia mkataba," Donald Trump ameongeza.

Rais wa Marekani amebaini kwamba anataka kupunguza idadi ya askari wa Marekani kutoka kati ya 13,000 na 14,000 leo hadi 8,600.