PAKISTANI-MUSHARRAF-HAKI

Rais wa zamani wa Pakistani Musharraf ahukumiwa kifo

Rais wa zamani wa Pakistani Pervez Musharraf, mwaka 2013.
Rais wa zamani wa Pakistani Pervez Musharraf, mwaka 2013. AFP Photos/Aamir Qureshi

Rais wa zamani wa Pakistani Pervez Musharraf, aliyekimbili uhamishoni Dubai, amehukumiwa kifo kwa kosa la 'uhaini mkubwa,' redio ya serikali ya Pakistani imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu ni wa kwanza katika nchi ambayo jeshi mara nyingi huonekana kama liko chini ya kinga kwa mashtaka. Hukumu hiyo imetolewa bila kuwepo kwake mahakamani.

Hukumu dhidi ya rais wa zamani inahusiana na "uamuzi wake wa Novemba 3, 2007," amebaini wakili wake, Akhtar Shah.

Jenerali Pervez Musharraf, wakati huo Rais wa Pakistani, alizuia Katiba na kutangaza utawala wa dharura uliolenga kuongeza muhula wake. Ni hatua ambayo inamuweka hatiani Pervez Musharraf, uamuzi uliotolewa na mahakama maalum.

Musharraf ambaye hivi sasa anaishi uhamishoni Dubai, alimuondowa madarakani waziri mkuu wa wakati huo Nawaz Sharif katika mapinduzi ya kijeshi mwaka 1999 na kuwa mtu maarufu ulimwenguni baada ya kujiunga na vita dhidi ya ugaidi viilivyoongozwa na Marekani nchini Afghanistan

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Pakistan askari kuhukumiwa kwa kosa hilo, amesema mwandishi wetu wa Islamabad Sonia Ghezali. Kile anachoshtumiwa ni kuzuia Katiba ili aendelea kusalia madarakani. Kwa upande wake, wakili wake amesisitiza kwamba mteja wake hajafanya chochote kibaya.

Jenerali Musharraf amekuwa akiishi Dubai tangu 2016 na amekataa kujiwasilisha mbele ya mahakama hiyo, licha ya maagizo kadhaa.

Hukumu ya kushangaza

Wachambuzi wengine wanahoji uhalali wa hukumu hii, baada ya kesi ambayo ilidumu kwa miaka sita na wakati ambapo mshtakiwa hakusikilizwa.