ISRAELI-SIASA-USALAMA

Israeli: Gideon Saar ajaribu kumuangusha Benjamin Netanyahu

Gideon Saar mpinzani mkuu wa Benyamin Netanyahu katika uchaguzi ndani ya chama cha Likud.
Gideon Saar mpinzani mkuu wa Benyamin Netanyahu katika uchaguzi ndani ya chama cha Likud. AFP Photos/Jack Guez

Baada ya majaribio mawili ya kushindwa kuunda serikali, Benjamin Netanyahu amelazimika kuandaa uchaguzi ili kushikilia nafasi yake katika chama cha Likud. Uchaguzi unafanyika leo Alhamisi, Desemba 26.

Matangazo ya kibiashara

Hadi sasa kiongozi ambaye hana mpinzani katika mrengo wa kulia nchini Israeli, Waziri Mkuu Benjamin Ntanyahu, sasa anakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Gideon Saar.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu Jerusalem, Guilhem Delteil, Gideon Saar alianza kupiga hatua katika siasa kupitia chama cha Likud cha Benjamin Netanyahu.

Awali alikuwa katika chama kidogo cha Tehiya, kilichopinga mchakato wa amani na Palestina mwanzoni mwa miaka 90.

Leo ndani ya chama kikuu cha mrengo wa kulia, Gideon Saar anaendelea kupinga mikataba ya Oslo. "Mataifa mawili ni kukanganya watu," alisema wiki iliyopita.

Bw Saa anatetea kuundwa kwa "eneo la Palestina" litakalounganishwa na Jordan.

Kampeni ya Gideon Saar, Waziri wa zamani wa Benjamin Netanyahu pia iliangazia kuhusu 'Israeli kubwa', akimaanisha nchi huru kutoka Bahari ya Mediterranian hadi mpaka wa Jordan.

Hata hivyo wakosoaji wake wanaona kuwa Bw Saar hana na fasi ya kumpiku waziri  Benjamin Netanyahu.