MAREKANI-IRAN-SYRIA-USALAMA

Washington yafanya mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa Iran

Jeshi la Marekani limeendesha mashambulizi ya anga dhidi ya ngome tano za kundi la Hezbollah lenye mafungamano na serikai ya Tehran  nchini Iraq na Syria (picha ya kumbukumbu).
Jeshi la Marekani limeendesha mashambulizi ya anga dhidi ya ngome tano za kundi la Hezbollah lenye mafungamano na serikai ya Tehran nchini Iraq na Syria (picha ya kumbukumbu). Reuters/US Air Force/Senior Airman Matthew Bruch/Handout

Jeshi la Marekani limetekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za kundi moja la wanamgambo wenye mafungamno na serikali ya Tehran, na kuua wapiganaji kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

Operesheni hii inakuja siku mbili baada ya shambulio la roketi ambalo lilimuua kwa mara ya kwanza raia mmoja wa Marekani nchini Iraq.

Jeshi la Marekani limesema siku ya Jumapili liliendesha mashambulizi ya anga dhidi ya ngome tano za kundi la Hezbollah lenye mafungamano na Iran nchini Iraq na Syria.

Mashambulizi hayo yaliyotekelezwa "kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara ya kundi la Kataëb Hezbollah dhidi ya kambi za jeshi la Iraq zinazokaliwa na vikosi vya operesheni vinavyopambana dhidi ya wanajihadi9 Inherent Resolve), yatadhoofisha uwezo wa kundi hilo la Kataëb Hezbollah kutekeleza mashambulizi ya baadaye dhidi ya vikosi vya muungano, "msemaji wa Pentagon Jonathan Hoffman amesema katika taarifa.

Kati ya ngome hizo tano, tatu zinapatikana nchini Iraqi na mbili nchini Syria, ameongeza Jonathan Hoffman.

Hii imekuja, baada ya mauaji ya mkandarasi wa Marekani aliyeuawa katika kambi ya jeshi nchini Iraq.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, ameishtumu serikali ya Iran kwa kutumia waasi wake kwa kuhusika pia katika mauaji hayo.