IRAQ-MAREKANI-MAANDAMANO-USALAMA

Waandamanaji wenye hasira waondoka mbele ya ubalozi wa Marekani Baghdad

Askari wa Marekani wakiwa juu ya paa la ubalozi wa nchi hiyo, Baghdad, Januari 1.
Askari wa Marekani wakiwa juu ya paa la ubalozi wa nchi hiyo, Baghdad, Januari 1. AHMAD AL-RUBAYE / AFP

Waandamanaji jijini Baghdad nchini Iraq wameondoka mbele ya Ubalozi wa Marekani, baada ya kuandamana kwa siku mbili, kuishtumu Marekani kwa kutekeleza shambulizi ya angaa dhidi ya kundi la waasi linaloongozwa na Kataib Hezbollah na kusababisha vifo vya watu 25.

Matangazo ya kibiashara

Wakiwa wamejihami kwa mawe na kuyaweka mbele ya Ubalozi huo, maelfu ya waandamanaji hao waliishumtumu pia Marekani kwa hatua yake ya kutangaza kuwa itawatuma wanajeshi zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Licha ya maandamano hayo, hakuna aliyejeruhiwa ndani ya ubalozi wa Marekani na shughuli zilionekana kuendelea kama kawaida.

Marekani imeishtumu Iran kuchochea maandamano hayo na kuonya kuchukua hatua, lakini baadaye rais Trump alinukuliwa akisema hataki vita na Iran.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo, ambaye alikuwa amepanga ziara nchini Ukraine, ameiahirisha ili kuendelea kufuatilia kinachotokea nchini Iraq.

Waandamanaji hao ni wafuasi wa kundi la waasi la Iran ambalo linatekeleza shughuli zake nchini Iraq.