MAREKANI-IRAN-IRAQ-USALAMA

Afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran auawa katika shambulizi la Marekani

Mkuu wa jeshi la Walinzi wa Mapinduzi wa Iran Jenerali Qasem Soleimani Oktoba 1, 2019 huko Tehran, Iran.
Mkuu wa jeshi la Walinzi wa Mapinduzi wa Iran Jenerali Qasem Soleimani Oktoba 1, 2019 huko Tehran, Iran. AFP Photos/Khamenei.IR via Handout

Mkuu wa jeshi la Walinzi wa Mapinduzi wa Iran Soleimani na kiongozi wa wanamgambo wa Iraq, Abu Mahdi al Mouhandis, wameuawa katika shambulizi la Marekani dhidi ya msafara wao kwenye uwanja wa ndege wa Baghdad.

Matangazo ya kibiashara

entagon imethibitisha kwamba Marekani imefanya shambulizi la anga lililo muua Jenerali Qassem Soleimani, ikisema kwamba imetaka kuishawishi Iran kwa mpango wowote wa shambulizi.

"Kwa kutii amri ya rais, jeshi la Marekani limechukua hatua madhubuti za kulinda wafanyakazi wa Marekani nje ya nchi kwa kumuua Qassem Soleimani," Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema katika taarifa.

Taarifa ya Wizara ya ulinzi inabaini kwamba "Qassem Soleimani alikuwa ameandaa mipango ya kushambulia wanadiplomasia na askari wa Marekani katika ukanda huo."

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka makundi matatu ya askari wa ziada wa Iran, roketi tatu zimerushwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baghdad, na kuua wapiganaji wao watano na "wageni" wawili.

Jenerali Soleimani alikuwa mmoja wa vigogo wa vikosi vya jeshi la Iran, nchini na nje ya nchi. Alikuwa akiongoza operesheni za kikosi cha ulinzi wa taifa nchi ya nchi, haswa nchini Syria na Iraq, na alikuwa na jukumu kubwa katika ushawishi mkubwa kwa Iran katika Mashariki ya Kati.