MAREKANI-IRAQ-USALAMA-USHIRIKIANO

Jeshi la Marekani latangaza "kimakosa" kujiandaa kuondoka Iraq

Marekani ina wanajeshi 5,200 nchini Iraq (picha ya kumbukumbu).
Marekani ina wanajeshi 5,200 nchini Iraq (picha ya kumbukumbu). SABAH ARAR / AFP

Baada ya uamuzi uliopitishwa na Bunge la Iraq kutaka kufukuzwa kwa wanajeshi wa kigeni,nchini humo,  jeshi la Marekani limetangaza "kimakosa", kwamba linajianda kuondoka nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Barua hiyo imesainiwa na Jenerali William H. Seely, kamanda wa operesheni za jeshi la Marekani nchini Iraq.

Katika barua hiyo, ambayo shirika la habari la AFP limepata kopi, Jenerali William H. Seely amembainishia kiongozi namba mbili wa jeshi la Iraq "kuweka sawa" vikosi vya muungano dhidi ya makundi ya kijihadi kwa lengo la "kuondoka Iraq kwa njia salama na madhubuti".

"Tunaheshimu uamuzi wenu ambao unatuagiza kuondoka Iraq," imeongeza barua hiyo.

Lakini saa chache baada ya tangazo hilo, mkuu wa majeshi ya Marekani amebaini kwamba tangazo hilo limepitishwa kimakosa. "Ilikuwa mradi wa ( barua) isio sainiwa, "iliyotumwa kwa baadhi ya viongozi wa jeshi la Iraq kwa sababu askari wengi wa Marekani walionekana katika maeneo mbalimbali nchini Iraq katika siku za hivi karibuni, Jenerali Mark Milley amewaambia waandishi wa habari. "Ni kosa lililofanywa kwa nia njema", ameongeza Jenerali Mark Milley.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Mark Esper amekanusha madai kuwa majeshi yake yanataka kuondoka Iraq, baada ya barua kutoka kwa jenerali wa Marekani kupendekeza waondoke.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Mark Esper amesema Marekani inakusanya wanajeshi wake, lakini haiondoki Iraq. "Hakuna uamuzi ambao umechukuliwa kuondoka Iraq. Mwisho, "Waziri wa Ulinzi wa Marekani amesema. "Barua hii haihusiani na hali yetu ya leo".