IRAN-MAREKANI-IRAQ-USALAMA

Rais wa Iran kulihutubia taifa baada ya mashambulizi dhidi ya askari wa Marekani

Rais wa Iran Hassan Rohani.
Rais wa Iran Hassan Rohani. HO / Iranian Presidency / AFP

Rais wa Iran, Hassan Rohani anatarajia kulihutubia taifa Jumatano wiki hii, hotuba ambayo itarushwa hewani moja kwa moja kwenye televisheni ya serikali, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Matangazo ya kibiashara

Hotuba hiyo inakuja saa chache baada ya jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kurusha makombora kadhaa dhidi ya kambi mbili za jeshi zinazotumiwa na Marekani nchini Iraq.

Pentagon inasema kuwa karibu kambi mbili zilishambuliwa, mjini Irbil na Al Asad.

Tayari baadhi ya wananchi wa Iraq wamebaini kwamba mashambulizi hayo ya iran nchini Iraq yanavunja uhuru wa nchi yao.

Runinga ya kitaifa ya Iran imetangaza kuwa shambulio hilo ni la kulipiza kisasi mauaji ya kamanda mkuu Qasem Soleimani aliyeuawa katika shambulio la ndege isiyokuwa na rubani mjini Baghdad, kufuatia agizo la rais wa Marekani Donald Trump.

Kuuwawa kwa Soleimani Januari 3 kulizorotesha uhusiano kati ya Iran na Marekani.

Jenerali Soleimani - alikuwa kiongozi wa oparesheni ya kijeshi ya Iran katika eneo la mashariki ya kati - lakini serikali ya Marekani ilimuona kuwa gaidi, ambaye alihusika na vifo vya mamia ya wanajeshi wake na kwamba alikuwa akipanga shambulio "hatari".