IRAQ-SYRIA-IS-USALAMA

Kiongozi mkuu wa IS athibitishwa

Bendera ya kundi la Islamic State kwenye barabara nchini Iraq.
Bendera ya kundi la Islamic State kwenye barabara nchini Iraq. REUTERS/Stringer/Files

Kulingana na gazeti la "The Guardian", kiongozi mpya wa kundi la Islamic State anaitwa Amir Mohammed Adbul Rahman al-Mawli al-Salbi. Yeye ni mmoja wa maveterani wa kundi hili na mmoja wa watu wenye msimamo mkali wa kidini.

Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa, anajulika kwa jina la kivita. Wakati huu, idara za ujasusi zinahakikisha kuwa tayari zimemtambua, gazeti la kila siku la Uingereza The Guardian limebaini.

Amir Mohammed Adbul Rahman al-Mawli al-Salbi ni msomi. Alihitimu Chuo Kikuu cha Mosul nchini Iraq, na alisoma sheria za dini.

Kulingana na gazeti la The Guardian, alionekana akitoa hoja za kidini kwa kuonyesha mateso yanayofanywa na wanajihadi. Kama mauaji ya watu na utumwa kwa jamii ya watu Yezidis au sera ya ugaidi inayoendeshwaa dhidi ya Wakristo katika bonde la Ninawi kuanzia Agosti 2014.

Inasemekana kwamba Al-Salbi alizaliwa kutoka familia ya asili ya Turkmen huko Tal Afar, kaskazini mwa nchi. Tarehe yake halisi ya kuzaliwa haijulikani, lakini yeye ni sehemu ya kizazi cha zamani.

Yeye ni mmoja wa waanzilishi wa kundi la IS, nguzo ya kundi hili, ambaye alikutana na Abu Bakr al-Baghdadi gerezani. Miaka kumi na tano iliyopita, walizuiliwa mahali pamoja na vikosi vya Marekani.

Marekani imetenga dola milioni tano kwa atakayemkamata au kumuua Amir Mohammed Adbul Rahman al-Mawli al-Salbi.