MAREKANI-MASHARIKI YA KATI-AMANI

Mpango wa amani wa Trump Mashariki ya Kati wapingwa Gaza

Maelfu ya watu wameingia mitaani katika mji wa Gaza kupinga mpango wa amani ambao Washington inatarajia kuzindua Jumanee wiki hiii. Kwa mujibu wa Marekani mpango huo unalenga kumaliza mzozo kati ya Israeli na Palestina lakini tayari umekataliwa na Wapalestina.

Wapalestina waandamana Januari 28, 2020 huko Gaza, kabla ya kutangazwa kwa mpango wa amani wa Marekani Mashariki ya Kati.
Wapalestina waandamana Januari 28, 2020 huko Gaza, kabla ya kutangazwa kwa mpango wa amani wa Marekani Mashariki ya Kati. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wamechoma matairi, bendera za Marekani na picha za rais wa Marekani, Donald Trump, huku wakiimba "mpango huo hautofaanikiwa."

Huko Rafah, Kusini mwa Ukanda wa Gaza, waandamanaji walibebelea bendera za Palestina, huku wengine wakichoma picha za Donald Trump.

Mikusanyiko pia inatarajiwa katika miji ya Nablus na Ramallah katika Ukingo wa Magharibi, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na walowezi wa Kiyahudi tangu mwaka 1967, na yanatarajiwa kuendelea usiku kucha.

Jumatatu wiki hii rais Trump alimpokea 'rafiki' yake, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na kiongozi wa upinzaji nchini Israeli Benny Gantz huko Washington, ambao wote wanadai mpango huo ni "wa kihistoria."