Pata taarifa kuu
SYRIA-UTURUKI-URUSI-USALAMA

Uturuki yaapa kukabiliana na vikosi vya Bashar Al Assad

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan avionya vikosi vya Bashar Al Assad ikiwa vitaendelea na mashambulizi katika Mkoa wa Idlib.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan avionya vikosi vya Bashar Al Assad ikiwa vitaendelea na mashambulizi katika Mkoa wa Idlib. Turkish President Tayyip Erdogan speaks during an interview with

Uturuki haitokubali vikosi vya Bashar Al Assad Assad kusonga mbele katika Mkoa wa Idlib, rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Jumanne wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limekuja saa chache baada ya vifo vya askari saba wa Uturuki na raia mmoja katika shambulio lililotokea katika mkoa huo wa Kaskazini Magharibi mwa Syria. Shambulio ambalo limedaiwa kutekelewza na vikosi vya Bashar al Assad.

Akiongea katika ndege iliyokuwa ikimrudisha kutoka Ukraine, rais wa Uturuki, akinukuliwa na kituo cha CNN nchini Uturuki, ameongeza kuwa haikuwa lazima kwa Uturuki kujiweka katika hali ya "mzozo mkubwa" na Urusi kuhusu matukio ya hivi karibuni nchini Syria.

Ankara na Moscow, ambao wanaunga mkono kambi za mahasimu katika mzozo wa Syria, watajadili maswali haya "bila hasira," Recep Tayyip Erdogan amesema.

Mkoa wa Idlib ndio ngome ya mwisho ya wapinzani wa serikali ya Bashar Al Assad. Vikosi vya serikali vinaendesha mashambulizi kabambe kwa usaidi wa ndege za kivita za Urusi kwa lengo la kuudhibiti mkoa huo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.