SYRIA-UTURUKI-USALAMA

Ankara yaonya Damascus, helikopta ya serikali yadunguliwa

Askari wa serikali ya Syria wamepelekwa karibu na barabara kuu ya M5 katika mkoa wa kusini wa Aleppo, Februari 10, 2020.
Askari wa serikali ya Syria wamepelekwa karibu na barabara kuu ya M5 katika mkoa wa kusini wa Aleppo, Februari 10, 2020. © AFP

Ankara imetoa onyo kali kwa Damascus Jumanne wiki hii baada ya vifo vya askari wake watano Kaskazini Magharibi mwa Syria, ambapo marubani wawili wa vikosi vya serikali wamepoteza maisha katika ajali ya helikopta yao baada ya kufyatuliwa kombora na vikosi vya Uturuki.

Matangazo ya kibiashara

Vitisho vya Uturuki, ambayo inaunga mkono makundi ya waasi na ambayo ina ngome za kijeshi katika mkoa huo, vimekuja wakati vikosi vya vya serikali ya Syria vinaendelea kusonga mbele katika uwanja wa mapigano baada ya kuweka kwenye himaya yao barabara kuu muhimu.

Watu wapatao 700,000 walitoroka makaazi yao kufuatia mashambulizi yaliyozinduliwa mwezi Desemba na serikali na mshirika wake Urusi katika mkoa wa Idleb, Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHa, imeonya.

Siku ya Jumatatu jioni, Ankara ilitangaza kwamba "imeangamiza" - bila kutoa maelezo zaidi kuhusu matumizi ya neno hilo. Wiki moja iliopita, mapigano yaligharimu watu ishirini katika kambi zote mbili.

Jumanne asubuhi, helikopta ya jeshi la Syria ilidunguliwa kwa kombora lililofyatuliwa na vikosi vya Uturuki Kusini Mashariki mwa mji wa Idleb, kulingana na Shirika la Haki za Binadamu la Syria (OSDH).

Ankara imethibtisha "tukio hilo", bila kukiri kuwa ilihusika.

Mwandishi wa shirika la Habari la AFP anasema ameona miili ya marubani wawili na mabaki ya helikopta hiyo kwenye eneo la ajali.