AFGHANISTANI-MAREKANI-USALAMA

Afganistani: Marekani kusaini mkataba na Taliban Februari 29

Marekani na kundi la wanamgambo wa Taliban wanatarajia kutia saini mkataba Februari 29 ikiwa kupungua kwa machafuko kuanza Jumamosi na kudumu wiki moja, hali ambayo itakuwa hatua ya kihistoria kwa mazungumzo ya amani nchini Afghanistan baada ya miaka 18 ya vita.

Raia watoroka makazi yao kufuatia mashambulizi yaTaliban katikati mwa jiji la Kunduz, Afghanistan, Agosti 31, 2019.
Raia watoroka makazi yao kufuatia mashambulizi yaTaliban katikati mwa jiji la Kunduz, Afghanistan, Agosti 31, 2019. REUTERS / Stringer
Matangazo ya kibiashara

Marekani ilikuwa ilitoa kama moja ya masharti kwa Taliban kupunguza mashambulizi nchini Afghanistan kabla ya kufikia mkataba huo.

"Mara tu (machafuko yatapungua), Marekani haitosita kutia saini kwenye mkataba na Taliban," amesema Mike Pompeo katika taarifa iliyotolewa baada ya ziara yake nchini Saudi Arabia.

"Tunajiandaa kwa utiaji saini huo Februari 29, " ameongeza Waeiri wa Mashauriano ya Kigeni aw Marekani.

Makubaliano yanaitaka Marekani kuondoa vikosi vyanchini Afghanistan, badala yake Taliban wahakikishe wamelinda usalama vilivyo.

"Baada ya mazungumzo marefu, (pande hizo mbili) zilikubali kusaini makubaliano yaliyokamilishwa mbele ya waangalizi wa kimataifa (...) mnamo Februari 29," Taliban imethibitisha katika taarifa.