SAUDI ARABIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Shughuli za kidini kwa wageni zasitishwa kwa muda Saudia Arabia

Saudi Arabia imeamua kusitisha "kwa muda" safari za kidini nchini humo.
Saudi Arabia imeamua kusitisha "kwa muda" safari za kidini nchini humo. Reuters

Saudi Arabia imeamua kusitisha kwa muda shughuli zakidini kwa Waislamu kutoka nchi za kigeni nchini humo. Mahujaji kutoka nchi za kigeni pia wamepigwa marufuku kuingia katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.

Matangazo ya kibiashara

Riyadh inataka "kuzuia maambukizi ya virusi vya Covid-19 katika nchi hiyo ya kifalme.

Serikali ya Saudia imeamua "kutia mariufuku kwa muda dhidi ya Waislamu kutoka nchi za kigeni ambao huingia kila mwaka nchini humo kutekeleza ibada za Umra na kutembelea Msikiti wa Mtume," wizara ya mambo ya nje imesema katika taarifa.

Pia kutembelea Msikiti wa Madina pia ni marifuku, taarifa hiyo imeongeza.

Wizara ya mambo ya nje ya Saudia inasema marufuku hiyo ni ya muda - lakini wizara hiyo haijataja lini marufuku hiyo itaondolewa.

Ibada ya Umra, ambayo inavutia makumi ya maelfu ya Waislamu kwenda Makka kila mwezi, ni Hija ambayo inaweza kufanywa wakati wowote wa mwaka. Wakati Hija ni ibada ambayo inaweza kutekelezwa tu kwa tarehe maalum kwenye kalenda ya mwezi ya Kiisilamu. Mwaka huu, ibada ya Hija itatekelezwa kati ya mwisho wa mwezi wa Julai na mwanzoni mwa mwezi Agosti.

Saudia pia imewapiga marufuku watu kutoka nchi zilizokumbwa na virusi hivyo kuingia nchini humo.