SYRIA-UTURUKI-USALAMA-SIASA

Syria: Ankara yajibu baada ya vifo vya askari wa Uturuki

Wapiganaji wa Syria wanaoungwa mkono na Uturuki wanaendesha kifaru katika mji wa Saraqib, mashariki mwa Jimbo la Idleb, Kaskazini Magharibi mwa Syria, mnamo Februari 27, 2020.
Wapiganaji wa Syria wanaoungwa mkono na Uturuki wanaendesha kifaru katika mji wa Saraqib, mashariki mwa Jimbo la Idleb, Kaskazini Magharibi mwa Syria, mnamo Februari 27, 2020. Bakr ALKASEM / AFP

Uturuki imetekeleza mashambulizi ya naga usiku Alhamisi kuamkia Ijumaa dhidi ya ngome za serikali ya Bashar al-Assad kwa kulipiza kisasi vifo vya askari 33 wa Uturuki katika mkoa wa Idleb (Kaskazini Magharibi mwa Syria), amesema rais wa Uturuki.

Matangazo ya kibiashara

"Ngome zote zinazojulikana za serikali ya (Syria) zimeteketezwa kwa moto na vikosi vyetu vya ardhini na wanaanga," mkurugenzi wa mawasiliano wa rais, Fahrettin Altun, amesema katika taarifa.

Mashambulizi haya yanakuja baada ya vifo vya askari wasiopungua thelathini na tatu katika mashambulizi ya anga yaliyoendeshwa na vikosi vya serikali ya Syria katika mkoa wa Idleb, kwa mujibu wa Ankara.

Ni moja ya mashambulio mabaya kabisa kuwahi kukumba jeshi la Uturuki katika historia yake ya hivi karibuni.

"Askari wetu mashujaa watalipiza kisasi," Bwana Altun amesema.

Afisa huyo wa Uturuki pia ametolea wito jamii ya kimataifa, pamoja na Urusi na Irani, washirika wa karibu wa Damascus, "kuchukua jukumu lao" "ili kukomesha uhalifu dhidi ya binadamu unaofanywa na serikali".