IRAQ-SIASA-USALAMA

Iraq: Waziri Mkuu aliyeteuliwa ajiuzulu

Rais Barham Salih ataanza mashauriano ya kuchagua mgombea mpya ndani ya siku 15, shirika la habari la serikali limetangaza.
Rais Barham Salih ataanza mashauriano ya kuchagua mgombea mpya ndani ya siku 15, shirika la habari la serikali limetangaza. AHMAD AL-RUBAYE / AFP

Waziri Mkuu wa Iraq aliyeteuliwa, Mohammed Allaoui, amejiuzulu wadhifa wake, na kushtumu vyama vya siasa kwa kuzuia mchango wake na kuchochea mgogoro nchini.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu unakuja saa kadhaa baada ya bunge kukataa kupitisha serikali yake mpya.

Mtangulizi wake, Adel Abdel Mahdi, alijiuzulu mwishoni mwa mwezi Novemba kufuatia maandamano makubwa ya raia, baada ya kuzuka makabiliano makubwa kati ya vyama vya Kishia vinavyomuunga na vile vinavyompinga.

Rais Barham Salih ataanza mashauriano ya kuchagua mgombea mpya ndani ya siku 15, shirika la habari la serikali limetangaza.