SYRIA-UTURUKI-URUSI-USALAMA-SIASA

Jeshi la Syria ladhibiti Saraqeb, Erdogan aitishia Ulaya

"Vikosi vya serikali ya Syria vikisaidiwa na jeshi la wanaanga la Urusi vimedhibiti eneo la kimkakati la Saraqeb," shirika la haki za binadamu Syria, OSDH limeliambia shirika la Habari la AFP.
"Vikosi vya serikali ya Syria vikisaidiwa na jeshi la wanaanga la Urusi vimedhibiti eneo la kimkakati la Saraqeb," shirika la haki za binadamu Syria, OSDH limeliambia shirika la Habari la AFP. Muhammad HAJ KADOUR / AFP

Vikosi vya utawala vya Damascus vinadhibiti tena Saraqeb, tangu Jumatatu Machi 2. Saraqeb ni eneo la kimkakati nchini Syria. Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, anatarajiwa kuzuru Moscow, Alhamisi Machi 5.

Matangazo ya kibiashara

Recep Tayyip Erdogan anatarajia kupata mkataba wa kusitisha mapigano kutoka kwa mwenzake wa Urusi Vladimir Putin. Recep Tayyip Erdogan anaendelea kuongeza shinikizo na kutishia kufungua mipaka yake kuwaruhusu wahamiaji na wakimbizi kutoka Syria wanaotafuta hifadhi katika nchi za Umoja wa Ulaya.

Jeshi la Syria liliingia Saraqeb Jumatau wiki hii, eneo ambalo linapatikana kwenye karibu na barabara mbili muhimu, Kusini Mashariki mwa mji wa Idleb. Saraqeb imedhibitiwa mara kadhaa katika wiki za hivi karibuni vikosi vya serikali, na baadaye makundi ya waasi kwa msaada wa Uturuki wiki iliyopita na sasa hivi imerudi kudhibitiwa na vikosi vya serikali ya Bashar Al Assad.

Urusi imetangaza kwamba vitengo vya Askari jeshi vimepelekwa Saraqeb, hali ambayo inaonyesha kuwa sasa Moscow inadhibiti eneo hilo.

Kulingana na shirika la Haki za binadamu nchini Syria, OSDH, askari zaidi ya 90 wa serikali wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Uturuki tangu siku ya Ijumaa pamoja na wapiganaji 10 wa Hezbollah.

Mkutano kati ya marais wa Urusi na Uturuki umepangwa kufanyika Alhamisi, Machi 5 huko Moscow. Recep Tayyip Erdogan amesema atataka vita visitishwe nchini Syria.

Vladimir Putin na Recep Tayyip Erdogan wanaunga mkono pande hasimu nchini Syria, lakini wameweza kuongea na hata kushirikiana katika miaka ya hivi karibuni.