MAEKANI-AFGHANISTAN-TALIBAN-SIASA-USALAMA

Afganistan: Trump aongea na kiongozi wa Taliban

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema mazungumzo kati yake na kiongozi wa kisiasa wa Taliban Jumanne wiki hii yamekuwa mazuri na ya kuridhisha.

Jumanne wiki hii, rais Donald Trump alizungumza kwa simu na kiongozi wa siasa wa Taliban, Mullah Abdul Ghani Baradar.
Jumanne wiki hii, rais Donald Trump alizungumza kwa simu na kiongozi wa siasa wa Taliban, Mullah Abdul Ghani Baradar. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

"Nimezungumza na kiongozi wa kisiasa wa Taliban kwa masaa kadhaa, na mazungumzo yamekuwa mazuri. Nina matumani nikitazama namna tulivyoongea, " amsema rais wa Marekani Donald Trump.

Jumanne wiki hii, rais Donald Trump alizungumza kwa simu na kiongozi wa siasa wa Taliban, Mullah Abdul Ghani Baradar.

Mazungumzo hayo yanakuja wakati wapiganaji wa Kiislamu wa Taliban wameanzisha tena mashambulizi dhidi ya vikosi vya Afghanistan.

Mashambulizi hayo dhidi ya kambi za jeshi yameibua masuali mengi kuhusu mkakati wa Taliban na nia yao ya kweli ya kufanya mazungumzo na serikali ya Kabul.

Rais wa Marekani ameonyesha matumaini yake kuhusu mchakato huo uanoendelea.

"Tulikuwa na mazungumzo mazuri," amesema Donald Trump.

Alipoulizwa ikiwa mazungumzo haya ya simu na Mullah Baradar, kiongozi mkuu wa ujumbe wa Taliban katika mchakato wa Doha, ni ya kwanza, Trump alikataa kutoa maelezo zaidi lakini amesisitiza kuhusu namna gani mazungumzo yao yalikuwa mazuri.

"Urafiki wangu na mullah ni mzuri sana," amesema rais wa Marekani. "Wanataka kumaliza machafuko," ameongeza.

"Nadhani sote tuna nia njema," amebaini Donald Trump, huku akikaribisha tena mchakato wa Doha. "Tumekuwa huko kwa miaka 20. Marais wengine walijaribu na wameshindwa kupata makubaliano ya aina hii."-

Hivi karibuni Marekani na Taliban walitia saini kwenye mkataba wa kihistoria ambao unaitaka Marekani kuondoa askari wake nchini Afghanistan.