AFGHANISTANI-MAREKANI-ICC-HAKI

ICC kufanya uchunguzi kuhusu uhalifu nchini Afghanistan

Wanajeshi wa NATO kutoka Marekani wakiwa katika eneo la ukaguzi katika mkoa wa Afghanistan wa Nangarhar, Julai 7, 2018
Wanajeshi wa NATO kutoka Marekani wakiwa katika eneo la ukaguzi katika mkoa wa Afghanistan wa Nangarhar, Julai 7, 2018 © AFP

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) wanatarajia kuamua leo Alhamisi juu ya ombi la mwendesha mashtaka kufungua uchunguzi kuhusu uhalifu dhidi ya binadamu na madai ya uhalifu wa kivita nchini Afghanistan, ikiwa ni pamoja mauaji yanayodaiwa kutekelewa na askari wa Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Mwezi Aprili majaji wa ICC, yenye makao yake Hague, walikataa kuruhusu uchunguzi wa uhalifu kama huo katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, wakisema hiyo "haitosaidia chochote mahakama" .

Uamuzi huo ulikuja wiki moja tu baada ya Mwendesha Mashitaka Mkuu kwenye Mahakama ya ICC, Fatou Bensouda, kunyimwa visa na Washington, ambayo ilikaribisha uamuzi huo ikisema ni "ushindi mkubwa".

Utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump, ulikuwa umepinga sana uchunguzi wa aina yoyote wa ICC nchini Afghanistan. Mahakama hiyo ya kimataifa ilianzishwa mnamo mwaka 2002 ili kuzima ukatili mbaya zaidi dunia.

Marekani, ambayo sio mwanachama wa ICC, ilitangaza katikati mwa mwezi Machi vikwazo vya kipekee dhidi ya mahakama hiyo ya kimataifa, na kumyima visa afisa yeyote "anayehusika moja kwa moja" kwa uchunguzi " dhidi ya wanajesi wa Marekani."

Mwendesha mashtaka Fatou Bensouda aalikataa rufaa dhidi ya uamuzi wa majaji mnamo mwezi Septemba. Uamuzi ambao ulikosolewa haraka na makundi mbalimbali ya wanaharakati wa haki za binadamu ambao walibaini kwamba ni pigo kubwa kwa "maelfu ya waathiriwa" wa mzozo wa Afghanistan.