SYRIA-UTURUKI-URUSI-USALAMA-SIASA

Syria: Marais wa Uturuki na Urusi wakubaliana kusitisha mapigano Idleb

Recep Tayyip Erdogan na Vadimir Putine huko Moscow, Machi 5, 2020.
Recep Tayyip Erdogan na Vadimir Putine huko Moscow, Machi 5, 2020. Pavel Golovkin/Pool via REUTERS

Urusi na Uturuki wamefikia makubaliano Alhamisi wiki hii kuhusu mkoa wa Idleb baada ya mkutano wa ana kwa ana huko Kremlin kati ya rais Vladimir Putin na mwenzake Recep Tayyip Erdogan.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Uturuki alikuwa amekuja Moscow kujadili mkataba wa kusitisha mapigano, hatua ambayo imeanza kutekelezwa usiku wa manane leo Ijumaa Machi 6, wakati katika uwanja wa mapambano hali imeendelea kuwa tete katika mkoa wa Idlib.

Mambo yatawekwa sawa ili kuhakikisha kwamba mapigano hayo yamekoma na mkataba unaheshimishwa, rais wa Uturuki amesema, huku akibaini kwamba majeshi yake yatajizuia kwa shambulio lolote kutoka vikosi vya Damascus.

Kwa upande mwingine Uturuki imeripoti kuwa imewauwa wanajeshi 21 wa Syria na kuharibu mifumo minne ya kufyatua makombora baada ya wanajeshi wake wawili kuuwawa.

Hata hivyo Shirika linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria (OSDH) limesema kumekuwepo utulivu kwenye maeneo mengi yaliyoandamwa na mapigano kwa wiki kadhaa zilizopita.

Alhamisi wiki hii wanajeshi wawili wa Uturuki waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa baada ya jeshi la Syria kuushambulia mji wa Idlib.