Benjamin Netanyahu na Benny Gantz kukutana kwa minajili ya kuunda serikali ya umoja
Imechapishwa: Imehaririwa:
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na mpinzani wake wa zamani Benny Gantz wanatarajia kuanza mazungumzo Jumatano wikii hii kuunda serikali ya umoja kabla ya usiku wa manane na kumaliza mzozo mrefu zaidi wa kisiasa nchini Israeli.
Baada ya miezi 16 ya serikali ya mpito, chaguzi tatu za wabunge, Bw. Netanyahu, 70, na Gantz, 60, walikutana Jumanne baada ya kupata muda wa nyongeza kutoka kwa Rais Reuven Rivlin kuunda muungano wa serikali.
Kwa idhini ya wabunge wengi baada ya uchaguzi wa wabunge wa Machi 2, Bw. Rivlin alikuwa amemwagiza Benny Gantz kuunda serikali ijayo. Lakini muda huo uliendelea hadi Jumatatu jioni na ulimalizika bila matokeo.
Bw.Gantz na Netanyahu hatimaye walisema wanajaribu kuunda serikali ya "umoja wa kitaifa na ya dharura" ili kukabiliana na janga la ugonjwa wa Covid-19 ambapo zaidi ya watu 12,000 wameambukizwa virusi vya ugonjwa huo, ambao umesababisha vifo126.
Rais Rivlin amewaongeza muda wa masaa 48, hadi usiku wa manane Jumatano wiki hii saa za Mashariki ya Kati (sawa na saa tatu usiku saa za kimataifa).
Siku ya Jumanne, timu zilizokuwa zikifanya mazungumzo kutoka chama cha Likoud, chama cha mrengo wa kulia cha Benjamin Netanyahu na chama cha "Bleu-Blanc", chama cha mrengo wa kati cha Bw. Gantz, zilihitimisha mkutano mwingine bila kufikia makubaliano.
Katika taarifa ya pamoja, pande hizo mbili zilisema watakutana tena Jumatano wiki hii baada ya kumalizika kwa Pasaka ya Kiyahudi, "kwa lengo la kuunda serikali ya dharura ya kitaifa".