ISRAELI-USALAMA-SIASA

Benjamin Netanyahu na Benny Gantz washindwa kuunda serikali ya muungano

Benjamin Netanyahu na Benny Gantz waendelea kuvutana na kushindwa kuunda serikali ya muungano.
Benjamin Netanyahu na Benny Gantz waendelea kuvutana na kushindwa kuunda serikali ya muungano. REUTERS

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mpinzani wake Benny Gantz wameshindwa kuunda serikali ya muungano ndani ya siku mbili walizopewa.

Matangazo ya kibiashara

Wapinzani hao walikuwa wameombwa na rais Reuven Rivlin kuunda serikali hiyo baada ya kutofanikiwa mara tatu kuunda serikali.

Mgogoro wa kiuchumi na kiafya uliosababishwa na kuzuka kwa janga la Covid-19 umeshindwa kumaliza mvutano wa kisiasa ambao tayari umefanya Waisraeli kushiriki katika chaguzi tatu za wabunge mwezi Aprili 2019, Septemba 2019 na Machi 2020.

Kukosekana kwa makubaliano kati ya wawili hao, Bunge linatarajia kuteua mgombea mpya, ambaye atakuwa na siku 14 kuunda serikali, ikishindikana, uchaguzi mpya wa wabunge utaitishwa.

Netanyahu na Gantz walitoa taarifa ya pamoja Alhamisi wiki hii wakisema wataendelea na mazungumzo baadaye leo.