ISRAELI-SIASA-USALAMA

Israeli: Netanyahu na Gantz wafikia makubaliano ya kuunda serikali ya dharura

Baada ya jitihada kadhaa, Benny Gantz (kushoto) na Benjamin Netanyahu wamefikia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja Jumatatu, Aprili 20.
Baada ya jitihada kadhaa, Benny Gantz (kushoto) na Benjamin Netanyahu wamefikia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja Jumatatu, Aprili 20. JACK GUEZ / AFP

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na hasimu wake wa zamani Benny Gantz wamefikia makubalio ya kuunda serikali ya umoja na ya dharura, na hivyo kumaliza mzozo mrefu wa kisiasa katika historia ya nchi hiyo wakati huu janga la Covid-19 likiendelea kuzua wasiwasi mkubwa duniani.

Matangazo ya kibiashara

Kufuatia kufikiwa makabaliano hayo Netanyahu aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa ametimiza ahadi ya kuipatia Israel serikali ya pamoja itakayofanya kazi ya kulinda maisha ya raia wa nchi hiyo.

Licha ya Netanyahu kupata ushindi mdogo dhidi ya Gantz katika duru tatu za uchaguzi mwaka uliopita, wanasiasa hao wote wawili hawakufanikiwa kuwa na wingi wa viti bungeni kuweza kuunda serikali.

Kufuatia kuzuka kwa janga la viruis vya corona, wito wa kuunda serikali ya pamoja uliongezeka nchini Israel kwa lengo la kuweka mikakati ya kudhibiti kuenea mzozo huo wa kiafya.

Chini ya makubaliano yaliyofikiwa nafasi katika baraza la mawaziri zitagawanywa kwa usawa kati ya chama cha Likud cha Netanyahu na kile cha mrengo wa kushoto cha Buluu na Nyeupe kinachoongozwa na Gantz.