AFGHANISTANI-TALIBAN-USALAMA

Taliban yafanya shambulio dhidi ya kambi ya jeshi Kusini mwa Afghanistan

Kundi la Taliban limekiri kuwa limetekeleza shambukio usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii dhidi ya kambi ya jeshi katika mkoa wa Helmand, Kusini mwa Afghanistan, ambapo karibu askari 150 wa vikosi vya jeshi na maafisa wa idara za ujasusi wanapiga kambi.

Vikosi vya usalama va Afghanistani vikipiga doria katika moja ya maeneo ya Mkoa wa Kunduz.
Vikosi vya usalama va Afghanistani vikipiga doria katika moja ya maeneo ya Mkoa wa Kunduz. REUTERS/Stringer NO RESALES. NO ARCHIVES
Matangazo ya kibiashara

"Askari wengi wa vikosi vya maadui wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio hilo," amesema Qari Yousuf Ahmedi, msemaji wa kundi hilo la wanamgambo wa Kiisilamu, katika taarifa .

Kulingana na afisa mmoja wa idara ya ujasusi aliyehojiwa na shirika la habari la Reuters, ambaye amesema ameona maiti 18, wapiganaji wa Taliban walilipua lori la jeshi kwa bomu walilokuwa wametega ardhini kwenye lango la kambi ya jeshi.

Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan imesema kwamba mlipuko ulitokea katika kambi hiyo, na kumjeruhi mtu mmoja.

Vikosi vya Afghanistan vimepata hasara kubwa katika miezi hii miwili iliyopita, licha ya kutiwa saini kwa makubaliano kati ya Marekani na Taliban Februari 29, ambayo yanatarajia kufungua njia ya mazungumzo ya amani kati ya Kabul na Waisilamu.