ISREAL-SIASA-USALAMA

Israeli: Mustakabali wa makubaliano ya Netanyahu na Gantz mikononi mwa Bunge na Mahakama

Wabunge nchini Israeli wanajadili leo Jumatano marekebisho ya hivi karibuni kuhusu makubaliano ya serikali ya umoja kati ya Waziri Mkuu anayemaliza muda wake, Benjamin Netanyahu na hasimu wake wa zamani Benny Gantz, ambayo inatarajiwa kupitishwa na bunge na Mahakama Kuu katika masaa yajayo.

Benny Gantz (kushoto) na Benyamin Netanyahu walifikia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja Jumatatu, Aprili 20.
Benny Gantz (kushoto) na Benyamin Netanyahu walifikia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja Jumatatu, Aprili 20. JACK GUEZ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Swali ambalo wengi wanajiuliza ni iwapo Israeli itapata nafuu baada ya kumalizika kwa mzozo wa kisiasa ambao ulikuwa ukiendelea tangu mwezi Desemba 2018 ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa uchaguzi mara tatu, hali ambayo haikupelekea kupatika kwa serikali moja.

Kutokana na hali ya mvutano na mgogoro wa kiafya uliosababishwa na janga la Corona, kiongozi wa upinzaji wakati huo Benny Gantz alipendekeza kuweka kando tofauti zao na kuunda serikali na mpinzani wake licha ya kushtakiwa kwa ufisadi, uvunjaji wa uaminifu na ubadhirifu.

Makubaliano hayo yaliwashangaza wanasiasa mbalimbali nchini Israel na kupingwa na mashirika mbalimbali yasio kuwa ya kiserikali hadi Mahakama Kuu, yakibaini kwamba Benjamin Netanyahu hawezi kuongoza serikali ijayo kwa sababu ya tuhuma zinazomkabili, na kwamba vifungu vya makubaliano haya vilikiuka sheria za msingi za Israeli, sawa na Katiba.

Wakati kesi hiyo ikisikilizwa kwa muda wa siku mbili mfululizo, Jumapili na Jumatatu wiki hii, majaji waliokuwa walivaa barakoa kama sehemu ya kukabiliana na maambukizi ya Corona, walipendekeza mabadiliko kadhaa kwenye makubaliano hayo.

Baada ya mapendekezo hayo, kambi za Benjamin Netanyahu na Benny Gantz zilirudi kwenye meza ya mazungumzo kwa madhumuni ya kurekebisha baadhi ya vipengele vya makubaliano ya awali.

Kwenye makubaliano hayo kuliongezwa maombi ya pande zinazopinga makubaliano ya Netanyahu na Gantz na kuamua kuwa serikali ijayo itakuwa serikali ya "umoja na ya dharura"ambapo Benjamin Netanyahu atahudumu miezi 18 kama waziri mkuu na akabidhiwe madaraka Benny Gantz ambaye pia atahudumu miezi 18, na kuonyesha mpango kuhusu kuunganishwa kwa eneo la Ukanda wa Magharibi kwa nchi ya Israel.

Hata hivyo, mwendesha mashtaka alikuwa ametaja kuepo na "matatizo muhimu (ya kisheria)" katika makubaliano ya Netanyahu na Gantz. Lakini saa chache zilizopita, na kwa kuzingatia marekebisho ya makubaliano hayo, ameonyesha Mahakama ya Juu zaidi nchini Israel kwamba haoni tatizo lolote linalozuia makubaliano hayo kupitishwa.