ISRAELI-NETANYAHU-SIASA-HAKI

Israeli: Mahakama Kuu yamruhusu Netanyahu kuunda Serikali

Mashtaka ya ufisadi dhidi ya Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu hayamzuii kuunda serikali, Mahakama Kuu ya Israeli imesema, uamuzi ambao unatoa nafasi ya kiongozi huyo wa chama cha Likud kusalia madarakani.

Benjamin Netanyahu aliyestakiwa mapema mwaka huu kwa ufisadi, udanganyifu na uvunjaji wa uaminifu, amekanusha mashitka hayo dhidi yake.
Benjamin Netanyahu aliyestakiwa mapema mwaka huu kwa ufisadi, udanganyifu na uvunjaji wa uaminifu, amekanusha mashitka hayo dhidi yake. REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Makundi ya upinzani yaliwasilisha mashitaka katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo yakishtumu makubaliano yaliyofikiwa mwezi uliopita kati ya Benjamin Netanyahu na hasimu wake mkuu Benny Gantz kwa lengo la kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kulindoa taifa hilo la Kiyahudi kwenye mgogoro wa kisiasa ambao haujawahi kutokea katika nchi hiyo.

Makundi hayo yalikuwa yamebaini kwamba mashtaka ya ufisadi, udanganyifu na uvunjaji wa uaminifu yanayomkabili Bw. Netanyahu, yangemzuia kuendelea kusalia madarakani.

Mahakama Kuu imebaini kwamba makubaliano hayo hayakiuki sheria na kwa hivyo imekataa kuyafuta, ikiondoa kizingiti muhimu kwa muungano wa serikali ambayo Netanyahu na Gantz wanapanga kurasimisha wiki ijayo.

Uamuzi wa mahakama unakuja wakati uchaguzi wa wabunge uliofanyika mara tatu chini ya mwaka mmoja, ambapo uchaguzi wa mwisho ulifanyika Machi 2, pande zote zilishindwa kupata viti vingi bungeni.

Mbali na mgogoro wa kisiasa, tangu mgogoro wa kiafya unaohusiana na ugonjwa Covid-19, uchumi wa Israeli umeendelea kudidimia.

Majaji 11 wa Mahakama Kuu wameeleza kwamba uamuzi wao huo "haupaswi kufasiriwa kama kupuuzia uzito wa mashtaka" dhidi ya Netanyahu, na kuongeza kwamba alikuwa na haki ya kudhaniwa kuwa hana hatia.

Kiongozi wa chama cha Likud, aliyestakiwa mapema mwaka huu kwa ufisadi, udanganyifu na uvunjaji wa uaminifu, amekanusha mashitka hayo dhidi yake. Kesi yake imepangwa kuanza Mei 24 mwaka huu.